Job 3:10-15


10 kwa sababu huo usiku haukunifungia
mlango wa tumbo la mama yangu,
ili kuyaficha macho yangu
kutokana na taabu.


11 a“Kwa nini sikuangamia wakati wa kuzaliwa?
Kwa nini sikufa nilipokuwa ninatoka tumboni?

12 bKwa nini pakawa na magoti ya kunipokea
na matiti ili nipate kunyonyeshwa?

13 cKwa maana sasa ningekuwa nimepumzika kwa amani.
Ningekuwa nimelala na kupumzika

14 dpamoja na wafalme na washauri wa dunia,
waliojijengea mahali ambapo sasa ni magofu,

15 epamoja na watawala waliokuwa na dhahabu,
waliozijaza nyumba zao kwa fedha.
Copyright information for SwhKC